𝐏𝐀𝐑𝐓 𝟏 – CHAGUA MWENYE ANAKUPENDA
Aje watu wangu! Tumerudi tena kupeleka weekie home straight.
Neema alimvutia Jojo pembeni akamwambia, “Uko na uhakika kweli unataka kuolewa na Joseph au unamskia huruma tu kwa mambo Jayden alimfanyia?” Jojo akamjibu, “Mum, niko sure kabisa. Nampenda Joseph, na si huruma. Jayden nilimpenda lakini Joseph ananipenda kwa kweli, na ni bora kuolewa na mtu anayekupenda kuliko yule unampenda peke yako.”
Jojo alijoin Amani wakajirusha kwa lovezone yao. Akampata Amani amezama kwa mawazo, akamwuliza, “Mbona unafikiria sana? Ama unajutia kuwa nami?” Amani akajibu, “Aa wapi, wewe ni everything. Nakupenda mbaya.” Kisha Amani akauliza Jojo kwa upole, “Uko ready kweli kuwa nami despite hali yangu?” Jojo akamjibu kwa ujasiri, “Mpaka mwisho, baby. For better for worse.” 😂❤️
Meanwhile, Naomi akiwa single bado, akasikia mlango unagongwa. Kumbe ni Richard 🤣🤣. Kumbuka Richard pia alikuwa ameachwa na Karen kabla hata story ianze 🤣. Naomi akashangaa, “Wewe huoni aibu kuja hapa?” Richard akasema, “Sikuja vibaya, nilitaka tu kukucheck.” Naomi akasema, “Actually umekuja poa. Nataka kuuza hii nyumba so utanisaidia na papers.” Richard akauliza, “Mbona unauza?” Naomi akasema, “Ni kubwa mno na kuna project nataka kufund na ninahitaji dough kubwa.”
Isabelle akiwa zake ndani, akashangaa kuona agent ana-take pics za nyumba yake. Kumbe Sharon yuko serious kuiuza. Isabelle akamfuata Sharon, “Mbona unaniwekea hivyo baada ya miaka yote?” Sharon akamjibu, “Si kwa ubaya, ni vile tu nahitaji pesa.” Isabelle akasema, “Shame on you!” Sharon akachemka, “Acha nicheze na wewe tu kwa sababu uko mzee. Ingekuwa mwingine, tungemalizana hapa!” 😤😤😤
Jojo akiwa na mamake, Rachael akaingia na prenup mkononi. Akampa Jojo, “Sign hii.” Jojo akamwuliza, “Hii ni nini?” Rachael akamwambia, “Prenup.” Jojo akashangaa, “Prenup ni nini? Ama ulikuwa campus kuosha sahani?” 😂😂😂
Neema ambaye anajua prenup, akamwambia Rachael, “Ya nini hii?” Rachael akasema, “Incaaaase Joseph afe, mali irudi kwetu—sisi familia yake—not kwa mgeni.” Neema akalipuka, “Acha matusi! Unaona mtoto wangu ni golddi...?”
Kwa wasiojua, prenup ni makubaliano kabla ya ndoa ya kwamba mali ya mtu haitaenda kwa mpenzi wake iwapo atafariki au watatengana. Rachael anajua Amani ana shares, so hataki Jojo arithi chochote.
---
𝐏𝐀𝐑𝐓 𝟐 – WEDDING YA KIROHO
Val alifika kwa Mark kumuona Joseph, lakini alijikuta anapewa invitation card ya harusi ya Jojo na Joseph. Val alikuwa amebeba chakula cha mgonjwa, lakini alibadilika kama transformer 😡 akaondoka straight hadi kwa Jayden.
Wakati huo, Naomi alijitokeza kwa Neema, eti anataka peace. Neema akamwambia, “Pole kwa yaliyopita.” Naomi akajifanya msosi, wakahug. But guess what? Naomi ana hidden agenda 🤣🤣. Akaondoka na invitation ya harusi.
Hapo Naomi akapiga Eddy simu, “Unajua mtoto wako anaolewa na Joseph na hujaitwa? Wah!” Eddy akaingia mguu mbili hadi kwa Mark usiku.
Mark akiwa kwa starehe zake, mlango ukagongwa. Kumbe ni Eddy. Eddy akaingia kama simba, “Naskia nonsense eti Jojo anaolewa na mtoto wako?” Mark akamwambia, “Relax bro, kaa chini tuelewane kama watu wa heshima.”
Eddy akawa mkali, “Mmeamua kusahau mimi ni babake Jojo?” Neema akamwambia, “Tulia bwana, Ian analala.” Mark akajaribu kubembeleza, lakini Eddy hakusikia. “Mbona Jojo anaolewa na mwanao?” akauliza.
Mark akasema kwa sauti ya pole, “Joseph ni mgonjwa, anaweza ondoka dunia muda wowote. Ndoto yake ya mwisho ilikuwa kuoa Jojo. Jojo akakubali.”
Eddy akabaki mdomo wazi, macho juu. Akaskia huruma, akakubali harusi iendelee. Jojo mwenyewe alikuja kumuuliza, “Nimepata gauni safi vipi?”
Yup, harusi inakuja. Hata kama hawajui kama Joseph atafika siku yenyewe akiwa hai. 😢😢
Nikimalizia… Val amefika kwa Jayden akamuliza, “Unakaa tu hapa wakati Joseph anaenda kuoa Jojo?” Jayden akasema, “Nifanye nini sasa?”
Val akamwambia, “You mean umekubali?” Jayden akamjibu, “Nimefanya makosa, nishap.