ππ„π„πŒπ€ πŸπŸ–π“π‡ π‰π”π‹π˜ π–π‘πˆπ“π“π„π 𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄𝐒

Neema Citizen TV Series 



𝐏𝐀𝐑𝐓 𝟏 

Mapenzi nayo huwa funny sana,Val anajua tu hapendwi na Amani but amekazana kabisa anataka kuenda kumuona. Sharon anamwambia hupendwi Val rudi kwa nyumba? But Val hataki kusikia..Punde si punde,Dancan akafika na gari fulani,hapo...akiringisha ufunguo,hadi Sharon akamuuliza wee,hii ni nini? Dancan akamwambia hii ni punda,kwani huoni hii ni gari 🀣🀣🀣🀣Dancan nikama njia zimefungua nyota imerudi tena amepata kazi.


Dancan ako happy sana,hadi ona venye anakaa kwa nyumba kama boss. Sharon alimuuliza biashara gani hizo umeanza? Dan akawaambia kila kitu,venye beshte yake alianza kuuza nyama na Dan amepewa tender ya kusuply nyama. Sharon anashindwa,na gari utakua unabebea nyama ama? Dancan akamwambia eeh,pickup ni yangu kabisa kabisa..Sharon akamuuliza so umenunua na how much? Dan akamwambia si hivyo hata,wamesema nipeane tu 450 so unaona zile 300k kwa account yetu nitoe nipeane..Sharon akashtuka,kwa nini,kwa sababu, ile account ndio walitumia kubuy manguo na sasa haina pesa🀣🀣🀣


Dancan alijam,akauliza Sharon,ni akili hauna ama,unaeza nunua nguo za 80k aje sasa? Sharon akamwambia yoh,hizo pesa ni zangu si zako. Dancan,nyota ikazimwa namna hivyo,pap!🀣🀣🀣🀣


Karen alikuja kukutana na Richard tena na Richy,ashajua sasa ashaangukia kadem karembo kama Karen,akamwambia sweetheart,so hii mapenzi yetu,tuifanyaje,iam ready for wedding 🀣🀣🀣Karen alicheka tu,akamuuliza wee mzee,umekaa tu ukaona msichana mrembo kama mimi naeza date mzee kama wewe hata nywele kwa kichwa pekee haikutaki? Richard akamuuliza so unamaanisha? Karen akamwambia I was just using you kurevenge for Naomi,mimi siezi kupenda kwa zile kiss nilikupea nafeel nimeshikwa na lyprosy,sijui river Jordan natoa wapi🀣🀣🀣🀣Richard,hakuamini! Imagine unaheartbreak mzee kama Richard wajameni.


Karen aliamka akaenda akaambia Richard type yako ni washosho,si kadem kama mimi..



Sasa sikiza,nyumba yenye Isabel na Babu wanakaa ndani kumbe huwa property za akina Dan..sasa ju wanataka pesa,Sharon aliamua kuja kuambia Isabelle, hii nyumba unakaa ndani si huwa yangu,so naiuza sijui mtafanyaje? Isabelle akamuuliza kichwa yako ni mzuri wewe,uuze nyumba ndio niende wapi? Sharon akamwambia penye utaenda uende uongee na bwanako,ama uende kuishi kwa Mark but nyumba yangu yenye unakaa ndani nauza.


Ahaa! Naomi wetu ashapona, Akitoka hosi alikutana na Richard,hapo. Richard kumuita,Naomi akamwambia please enda ita huyo Karen wako si mimi...Richard akamwambia sitaki kusikia hilo jina. Naomi akajua ooh ushapewa character development already 🀣🀣🀣🀣


𝐏𝐀𝐑𝐓 𝟐 

Good news, Amani ashapata nafuu hadi wamerudi nyumbani.


Rachael alihug Mark akimwambia ooh sijui mtoto wetu lakini Mark aliangalia tu kando,kisha Rachael akafanya makosa,akaambia Jojo asiwai onekana na mtoto wake lakini Jojo akamwambia wee pia usijifanye as if chenye ulifanya si kitu.


Rachael anajifanya sympathetic sana lakini Mark akamwambia wee na wewe Rachael,usijifanye mtakatifu hapa after chenye umejaribu kufanyia Jojo. Hapo ndio Rachael akajua,kumbe Mark ashakua briefed.


Amani hana usingizi,hadi alikuja akaambia akina Mark, hana usingizi ju ako na guilt sana..Mark akamuuliza guilt gani? Amani akamwambia mimi kuwa karibu na Jojo najua imeumiza sana mtu kama Jayden na sikutaka kuumiza mtu yeyote. Neema akaona ahaa at least ameomba msamaha lakini Amani akaambia Neema, mama Jojo, wuth due respect,I love your daughter sana..nampenda Jojo na ningependa sana niwe na yeye. Jojo kalikua hapo kameenjoy sana hadi kakauliza Amani,you mean it? Amani akamwambia yeah nakupenda..Jojo akamwambia so tunangpoja nini,lets get married. Hii yote walisema mbele ya wazazi wao. Mark,Neema na Rachael wamebaki kushtuka tu.


Baadae,Neema alikuja tu kuconfirm kwa Jojo kama she meant it..Jojo akamwambia yeah,iam serious and trust me on this mum. I love Amani.


Babu Jay na Isabelle wamekuja kutembelea akina Mark huku,its been long sana tangu waonane.



Manze Jayden ako soo down sana...amekuja kukaa peke yake analia tu,anawish babake angekua hata ingekua afadhali,ju hadi anaona because of love karibu amuue Amani,hadi anaona haina haja ya kuishi.


Upande wa Mark,Neema alikua amemuita Babu Jay awasaidie kuhusu hii issue ya Jojo kutaka kuoana na Amani. Babu akamuuliza kuna ugumu gani kwani? Neema akamwambia ni ju mimi na Mark ni wapenzi society itasemaje? Babu akamwambia sikiza, wewe na Mark ndio mnapendana na si society,so achana na society plus chenye wanasema,the same way unapenda Mark acha Jojo na Joseph waoane,hawahusiani kidamu kwa njia yoyote.


In short, Babu aliambia akina Neema, Jojo na Joseph wana haki ya kufendana venye tu wewe na Mark mnafendana. Sasa Rachael akisikia hivi anatamani kupasuka lakini apasuke ama abondeke, hali halisi ndio hivyo,Jojo anampenda Joseph,na Neema anampenda Mark.


Nimemaliza.

Post a Comment

Previous Post Next Post