𝐍𝐄𝐄𝐌𝐀 𝟕𝐓𝐇 𝐀𝐔𝐆 𝐖𝐑𝐈𝐓𝐓𝐄𝐍 𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄𝐒
Team Neema,usipite hii bila kuweka LIKE
𝐏𝐀𝐑𝐓 𝟏
Eish mapema kama hii sasa,Neema amekaa but kila saa anaangalia tu picha za mark,anashindwa mpenzi uko wapi? Neema alikaa akaona acha wafanye kitu maybe Mark atarudi,kitu gani? Aliambia akina Jojo waende wasafishe nyumba ya Mark maybe atarudi..Jojo wanashindwa,kwani mama yao amechizi ama kunaendaje😂😂😂but Neema ako serious sana😂😂😂wanaenda akuosha nyumba ya Mark.
Watuuuuuuuuuuuu! Mkufi ameamka tena haya 😂😂Kumbe Rachael alifaint tu, ndio anafenduka sasa,akauliza Isaac,wee kwani niko wapi? Isaac akamwambia uko kwa room yangu,ulianguka ukagonga kichwa. Rachael akamwambia shame on you,unadhani siezi kumbuka ni wewe ulinisukuma? Isaac akamwambia wewe ndio shame on you,umesahau ni wewe ulijileta hapa😂😂😂
Good thing,huku ni side ingine sasa, Neema alipigiwa simu na Sharon kumbe pia alitumana watu wakakuja kusafisha nyumba ya Mark.
Sharon wamerudi nyumbani bado amekasirikiana na Dan,sasa Dan akiuliza kitu,badala ya Sharon kujibu,anaambia Val aambie babake😂😂😂sikiza, Dancan akiuliza Sharon kuhusu supper,Sharon anaambia Val,aambie babake leo hakuna supper. Sharon akauliza Val kama ako na number za lawyer Richard mwenye? Val akauliza mamake,na hii miaka yako unataka kuachana na dad uende wapi? Sharon akamwambia ooh,iam still childred,mimi ni gen Z alah,kumi na nne supuu😂😂😂
Tufike kwa Jojo na Amani,wamekaa but Amani hana amani,ju hajui mamake ako wapi,hadi Jojo akimwambia kitu,Amani anamwambia iam just worried about my mum...Jojo akamuuliza ooh,after everything she has done? Amani akamwambia she is still my mum, lazima niwe worried.
Rachael aliamka akakuja straight hadi penye Amani ako. Amani kumuona akaona ile alama yenye alijigonga akauliza mamake wait,what happened ama ni Isaac alifanya hivi? Rachael akamwambia yeah,lakini Jojo akamwambia nini "yes you deserve it", Amani akajam akaambia Jojo wee mwanamke uchunge sana chenye unafungua kwa huo mdomo wako,this is my mum na ufikirie sana chenye unaongea 😂😂😂Yeah! Jojo,huyu ni bwanako anakupea msomo ukiongelea mamako😂😂
Woiye Neema,halali,hali anafikiria tu Mark. Hata hakuenda kwa accident scene kuona kama alirudi but anaomba tu Mark arudi,anamumiss sana. Neema anawish tu Mark akuje ju haezi bila yeye lakini punde si punde Neema akiwa amekaa,akashikwa kwa mabega,kuangalia,ahaa,yeeees one and only,Mark is back akiwa na bandage kwa mkono. Neema kwanza akadhani anaota ikabidi sasa amemshika Mark mwili mzima kuhakikisha tu ni yeye and yeah,,Mark is back, Kila mtu alikua happy sana.
𝐏𝐀𝐑𝐓 𝟐
Mark hata hawakulala,walikuja direct hadi polisi kuandika statement,akaulizwa kama kuna mtu wamekosana ama wako maadui,Mark akamwambia yeah, someone is after me na namjua.
Neema akanotice,kuna vitu Mark anaficha but Mark anajua kuna mtu anawatafuta.
Karen baada ya kuhanda Naomi alimwambia amtafutie pesa tena mingi sana,so ile balance yenye Naomi alibakisha kwa kuuza nyumba,aliletea Karen,ju angekataa kingeumana.
Sasa cheki,hivi ndio Karen alitaka,she has enough ya kutosha and they went away happy than ever na hivyo ndio Karen alirevenge kwa Naomi 😂😂kuna pesa kiasi Karen alichukua akaambia Job anapelekea mtu fulani. Tutakuja kuona ni nani ataletewa pesa.
Dan bado amejam ju Sharon ameshikilia msimamo wake,anataka divorce 😂😂😂
Na nikama Naomi na Richard wanarudiana sindio..ju leo Richard ameinvite Naomi leo baada ya kusikia ati atalala kwa hotel. Kisha Richard akauliza Naomi,hujafanyia akina Naomi anything ju najua sai wako na shida sana? Naomi akawaambia wako sawa,ile nyumba nilinunua niliwapea wakae ndani...Richard akashtuka akamwambia ah,kwani sikuhizi umechange,hukuangi hivyo? Naomi akamwambia nakuanga mzuri ni venye huwa sisemi. At this point,bado Richard na Naomi hawajui Mark alirudi. Ops kuna post nilieka nikasema Mark amerudi kama hajui Neema,niliwadanganya wakuu,,,it was just for fun.Mark is back the same Mark.
Punde si punde,Sharon akamcall Richard,akamuuliza atafika huku saa ngapi anataka amfanyie story ya divorce? Richard akamuuliza aah nikuje kufanya nini sina kazi huko? Sharon akamwambia haya,hukuji kuona Mark,amerudi. Naomi kusikia hivyo,akajua wah,kwisha.
Kumbe Mark,alishika number plates za lile gari lilimgonga,but hataki kuambia Neema,anacheza kichini chini alicall jamaa wake akamwambia amuangalilie mwenye hilo gari ni nani.
Rachael na yeye aliitwa na Isaac,waongee tutakuja kujua chenye waliongea.
Richard alikuja kuona Mark,akauliza yani Mark anarudi hamuezi niambia? Neema akamwambia ni venye ile furaha ya confusion. Richard anashindwa sana hadi anauliza Mark,wewe unakuanga driver mzuri,kuliendaje? Neema akaambia Richard,haikua ajali ya kawaida,someone knew what he/she was doing. Naomi akashtuka😂😂😂
Jojo pia alikua hapo,akasema basi ashajua mwenye alifanya lazima ni Isaac..Naomi akauliza Isaac ni nani?
Rachael aliingia kwa gari ya Isaac,akamuuliza,wee mwanaume unataka nini mimi after chenye ulinifanyia?